Naogopa. Tena naogopa sana. Maana kujaribu kumteta Lady Jaydee humu ndani ni kosa na kujitakia maisha mafupi. Yule mwandishi aliyejaribu 'kutoboa' kuwa mwanamuziki wa 'miondoko ya R&B' alikula 'ze sem pleti' na Meneja wake keshawekewa wanted. Du! hii hatari. Isingekuwa kuwategemea mabodigadi wangu, nisinge thubutu kusema lolote juu ya hili jambo. Sema nitatumia ujuzi wangu wa kijasusi kukwepa 'fatwa' yoyote itakayokuwa 'issued' na Lady Al-Jayzeera.

Hata hivyo mimi naona nimtetee Judith Wambura. Kwanza mimi ni shabiki wake (najikomba). Maana anaimba 'vizuri' sana (najikomba tena) kuliko hata Tina Turner (hapa nimezidisha). Pili, kwani akitoa vituuz kuna ubaya? Nyie mlitegemea nini? Wewe msichana unavihamu vyako na uko hapo bondeni, umepata dinner ya nguvu, umekunywa 'wine' na magoti yamekulegea utafikiri unaumwa 'romatizimu' halafu 'Meneja' wako uchwara anaanza mchezo mbaya wa kukushika kiuno au matako na kwa sababu umelewa, wewe unachekacheka ovyo tu kama mwehu anayehitaji kupandwa. 'Mafeeling' yanakuzidi na inabidi uishie naye bedirumu moja. Mimi katika kazi yangu ya ujasusi nimeshawahi hata kula sahani moja na adui mmoja wa kike. Ilibidi maana alikuwa mzuri sana na kuachia 'ngoma' eti kwa sababu ana bastola chini ya mto, waswahili wanasema ni uchoko huo! Kwa hiyo 'nili-risk'. Jaydee naye 'ka-risk' kama bina'adam tu, yakhe.

Lakini wazo moja linanijia. hivi 'Lady Jaydee' anajua kuhusu mapenzi salama? Atalala na wangapi? Leo 'meneja' uchwara kutoka bongo (Ruge Mutahaba), kesho ni 'Recording Executive' wa Sony Music Corporation. Atampatia vituuz pia? Na hapo katikati atakuwa ametoa vituuz kwa wangapi?

Wazo lingine linanijia vilevile, Hivi Lady J anajua maana ya kuwa kwenye 'jicho la umma'? Ukifikia katika sehemu hii basi ujue kila ulifanyalo litawekewa alama ya kuuliza. Ndiyo bei ya kujulikana. Hakuna kitu cha bure hapa duniani. Angekuwa msichana wa kazi kwa Bw. Viraj Sanjay nani angejali?

Wazo lingine la mwisho. Tanzania hivi sasa ni demokrasia. Watu wana haki ya kuuliza kama mtu maarufu ambaye anatakiwa kuwa mfano kwa vijana wa Tanzania anapokwenda kombo. Katika demokrasia tuna haki ya kukemea makosa na kueleza kwa uwazi. Kutishia wenzako kwa vile 'wametoboa' siri si kitendo kizuri. Tuko huru kusema lolote. Kama hutaki basi amua moja kati ya kujiheshimu au kutoka kabisa kwenye umaarufu!

Hao polisi wakimpata wanastahili nao kumfungulia mashataka. Kwa huyu mwanadada kumshambulia mtu kwa lugha ya matusi pamoja na kumtishia maisha mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Dina Ismail, ni kitendo cha aibu kwa mtu 'maarufu'. Akipatikana na hatia, adabu inayostahili itolewe. Na hakuna kutoa hongo au kumlipa mtu mwengine akufanyie adhabu hiyo!

Jaydee, nasubiri na mimi vitisho toka kwako. Unaweza kuniandikia powersbongo@yahoo.com au kunipigia simu ya satellite +9685 96738 378447. Aidha unaweza 'kudropu-bai' MI6 headquarters, Vauxhall Cross, London. Anwani ya posta: MI6 / SIS, PO Box 1300, London SE1 1BD, U.K.

Porojo -HOME