Mkapa, Tony Blair na Clinton walikuwa wamekaa barazani wanaongea. Mara mungu akatokea. Akawaambia kuwa atawapa wote nafasi ya kuuliza swali moja tu kila mmoja.

Blair: Oh God, nchi yangu itabadilika na kuwa nzuri zaidi kweli? Mungu: Siyo katika maisha yako. labda viongozi watatu wajao ndiyo wataweza kurudisha nchi hii ifikie ule wakati Uingereza ilipokuwa ikitawala dunia.

Clinton: My lord, God, nimeshastaafu, lakini nchi yangu itakaa ibadilike kweli? Ningependa watu waache kufuatilia maisha binafsi ya watu. Watu waache umbeya usiofaa. Na waislamu waache kutuchukia sisi wamarekani bure. Mungu: Siyo mwaka huu au ujao, wala siyo katika maisha yako wewe. Nchi yako labda baada ya marais wengine sita.

Mkapa: Mnyaaazi mungu muumba wa yote. Lini nchi yangu itabadilika na kuwa tajiri isiyotegemea misaada wala kutokuwa na viongozi wanaoibia wananchi?? Mungu: Siyo katika maisha yangu mimi!

Porojo Page -HOME