Salimuni Amri!!
Wazenji hatukuamini masikio yetu siku ile neshno egzekyutiv ilivyotugeuzia kibao. Na kilichonishangaza mimi zaidi ni jinsi nilivyoona watu wanatoka kikaoni wanacheka na kukumbatiana au kuonesheana dole gumba kwa "ushindi" wa maamuzi ya kamati hiyo. Yaani mijitu ya bara inakenua meno kwa kuzima harakati za wazenji kujiamulia mambo yao wenyewe?
Kabla sijaendelea na kilio changu naomba kwanza niwafafanulie wabara maana ya demokrasia. Hebu acheni mambo ya ajabu. Demokrasia ni kuheshimu matakwa ya watu. Matakwa yetu ni Salmini kuendelea kuongoza na siyo "kutawala" (maana wabara mnamwita mtawala wakati Mkapa mnamwita kiongozi).
Kama mnajidai kuwa kikatiba chenu cha CCM hakiruhusu "kutawala" mara tatu, basi kilichobaki ni sisi kujiundia tena chama chetu (kilichotukomboa kwenye mikono ya sultani) yaani Afro-Shiraz Party .
Huu muungano ni unafiki. Eti leo hii unasikia "wapinzani" wanaipongeza NEC kwa kuzima harakati za Zanzibar. Cheyo wa UDP anasema eti ni "ushindi" kwa watu wa Zanzibar na wa bara. Kesho wanalilia demokrasia zaidi!!! Unafiki mwengine ni ule wa CCM. Juzi juzi wamebadili katiba kujiongezea nguvu zaidi na kumpatia rais wao nguvu. Zanzibar tukitaka kufanya hivyo tunaonekana "wahuni" wa maskani.
![]() |
"Zanzibar tuachie wenyewe" |
CCM watajutia nafasi hii ya kubadili katiba. Wangekuwa wana akili wangekubali sisi wazenji tubadili katiba na Mkapa naye angepata fursa ya kubadili katiba baada ya 2005. Sasa hi ni sawa sawa na Mkapa mwenyewe kujizibia fursa.
Mkapa anaweza kufikiria itakuwa raisi kubadili katiba lakini atajuta nawaambieni kwa sababu huwezi kujua kama watapata idadi kubwa ya wabunge kama ilivyo sasa.
Mungu aibariki Zanzibar. Tunajua tumeshindwa ngwe hii lakini mambo hayajaishia hapo.
Note: This is an article contributed by Ali Zuberi Mohamed.
Suggestions welcomed at Powers.