Deobandism

'Deobandism is a puritanical Islamic movement that began in colonial India more than 100 years ago. Although few non-muslims have heard of it, their teachings form the basis of the Taliban's beliefs.' -- Luke Harding

 

Shule ya kidini ya Darul Uloom Deoband iliyoko kwenye mji wa Deoband, iko kama shule yoyote ile ya kawaida. Imejengewa ukuta mrefu mzuri na nje yake kuna wananchi wanafanya biashara zao kama kawaida. Wanawake wanavaa burqa na kuombaomba barabarani huku wanaume wanakunywa chai kwenye migahawa iliyojaa nzi wengi sana. Mji unafanana na Kabul.

 

Ndani ya shule hii yenye wanafunzi 3200, ndipo Taliban ilipozaliwa. Siyo miaka 10 iliyopita, bali miaka 130 iloyopita, tena chini ya mti. Deobandism inafuata sharia. Mwanamke awe muislamu au asiwe, anachapwa viboko katika mji huu kama anatoka nje bila burqa au anaongea na wanaume asiowajua. Wezi wanakatwa mikono, wanaoabudu sanamu nao wanakiona cha mtema kuni. Kuangalia sinema ni marufuku, labda taarifa ya habari.

 

Qasim, mzee mmoja anayedai aliyekuwepo wakati wa waiingereza, anasema siku zote watu wamekuwa wakiadhibiwa ipasavyo. Qasim anasema hawakutaka nchi ya Pakistani itenganishwe na India. Anamuita Jinnah (aliyeoongoza Pakistan kupata uhuru) msaliti mkubwa. Hata hivyo Qasim anasema Taliban walizidisha ukali wa mafundisho ya Deobandism. Angalau wao wanaruhusu kuangalia taarifa ya habari.

 

Hata hivyo wanafunzi wengi wa Deoband wanaisifu Taliban na wanasema walipaswa kupewa msaada katika vita yao dhidi ya 'kafiroon' Mmarekani na wenzake wa magharibi. Kwa nini wao hawakwenda huko kuwasaidia watalibani? Wana shughuli za kimasomo hivyo hawana muda kwenda kuungana nao! Huenda wanaogopa kukutana na kilichowakuta ndugu zao Taliban.

 

 

Porojo

Home

comments